NUNUA | UZA | PANGA NA KUPANGISHA

UZA HAPA KWA Tsh. 5000 TUU kwa SIKU 5, Contact: 0713522168

TANGAZO TOKA TANESCO..*TAARIFA KWA WATEJA WETU WA MKOA WA KINONDONI KUSINI* Kwa sasa tumefanikiwa kuunga umeme Wateja wetu waliokuwa wanapata umeme kutoka njia kubwa ya umeme ya *NORDIC1* sasa wanapata kutoka kituo chetu che Mbezi kupitia eneo la Goba Kwa wateja waliokuwa wanapata umeme kutoka line ya *NPRDIC2* mda si mrefu watapata kutoka line ya Segerea kupitia eneo la Kifuru. Maeneo mengine ya Chuo Kikuu, Magomeni na baadhi ya maeneo ya makongo na mburahati wanapata umeme kutoka Ilala Substation. **Maeneo yaliyobakia ya Changanyikeni, Viwanda vilivyopo mandela road pamoja na Bakresa Buguruni,*Tandale, Sinza.,Ubungo karibu na bus stand na shekilango na baadhi ya maeneo ya mburahati bado tunaendelea na juhudi za kuweza kuwapatia huduma kutoka vyanzo vingine.* Wataalamu wetu kutoka Ubungo Workshop bado wako kwenye eneo la tukio kwa uchunguzi na kurekebisha hitilafu iliyotokea ili umeme uweze kurudi kwenye hali yake. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wateja wetu lakini pia tuombe utulivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Kwa mawasiliano Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100 Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii: Mitandao ya kijamii Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,  Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/ IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO TANESCO MAKAO MAKUU APRILI 02, 2018

No comments:

Post a Comment

Popular Posts